Rais Xi Jinping kushiriki mkutano wa 23 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa SCO
2023-06-30 13:10:40| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying ametangaza kuwa kutokana na mwaliko wa Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, Rais Xi Jinping wa China atashiriki na kuhutubia kwa njia ya video Mkutano wa 23 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO).