Waziri wa viwanda na biashara wa Angola Victor Fernandes amesema Angola na China zina mustakabali mkubwa wa ushirikiano, na amezikaribisha kampuni nyingi zaidi za China kuwekeza nchini Angola.
Fernandes amesema hayo aliposhiriki katika Maonesho ya Tatu ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yanayofanyika mjini Changsha, China, ambayo yamechangia sana katika ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika. Anaona kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika umeleta faida kubwa na utaimarishwa zaidi katika siku za baadaye.
Pia anatarajia uwekezaji wa China utaweza kuisaidia Afrika kuongeza uwezo wake wa utengenezaji, ili kubadilisha malighafi kuwa bidhaa kamili na kuuzwa duniani.