CPC yaongoza ujenzi wa jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja
2023-06-30 13:34:59| CRI
Tarehe 1 Julai mwaka huu ni kumbukumbu ya miaka 102 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China CPC. Katika kipindi cha karne iliyopita, CPC kimewaongoza Wachina kufikia maendeleo ya kihistoria, na kuiendeleza China, iliyokuwa maskini na dhaifu, kuwa nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani. Wakati huo huo, katika mapambano ya muda mrefu ya pamoja na utafutaji wa maendeleo kupitia ushirikiano, China na Afrika zimeanzisha wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa kina, na kuchangia maendeleo ya pamoja ya pande hizo mbili.

 

"CPC kinapenda kufunzana kuhusu uzoefu wa utawala bora wa nchi na vyama vya siasa vya nchi za Afrika, kusaidiana katika kutafuta njia ya maendeleo inayoendana na hali ya taifa, kuimarisha ushirikiano wa kivitendo katika nyanja mbalimbali, na kuhimiza ujenzi wa Jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja." Mapema mwaka jana, Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere kilichojengwa na vyama sita rafiki vya Kusini mwa Afrika na kuungwa mkono na CPC kilizinduliwa nchini Tanzania, ambapo Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na Rais wa China Xi Jinping alituma barua ya pongezi.

 

Ikiwa ni alama muhimu ya urafiki na ushirikiano kati ya vyama vya kisiasa vya China na nchi za Afrika, Chuo cha Uongozi cha Nyerere kilichopewa jina la Hayati “Baba wa Taifa” Nyerere wa Tanzania kinajulikana kama “Reli ya TAZARA ya Kimawazo”. Katika miaka ya 1950 na 1960, Afrika ilikuwa jukwaa kuu la dunia kupinga ukoloni na kupigania ukombozi wa kitaifa. Viongozi wa kizazi kikongwe wa CPC walisimama upande wa maendeleo ya binadamu na haki ya dunia, na kujitahidi kadiri wawezavyo kutoa uungaji mkono wa kujitolea kwa nchi za Afrika. Hayati mwenyekiti Mao Zedong alipopokea wageni kutoka nchi za Afrika mwaka 1959, alipendekeza kwa ubunifu kwamba Waafrika wanapaswa kushughulikia masuala ya Afrika wao wenyewe, kutegemea nguvu zao wenyewe, na wakati huo huo kutafuta marafiki duniani, ambapo China bila shaka itaiunga mkono Afrika. Tangu wakati huo, China imesaidia katika ujenzi wa Reli ya TAZARA, ambayo inajulikana kama "Njia ya Uhuru" na "Njia ya Urafiki" na watu wa Afrika, kufungua njia kuu ya kiuchumi kusini mashariki mwa Afrika, jambo ambalo pia limejenga urafiki mkubwa wa kimapinduzi kati ya China na Afrika.

 

Katika miaka ya 1990, ingawa nchi za Afrika zimepata uhuru wa kitaifa, athari mbaya zilizotokana na utawala wa kikoloni hazijaondolewa, vita vya wenyewe kwa wenyewe vilitokea mara kwa mara, na uchumi ulikuwa mbaya, na hata Afrika iliitwa "bara lililosahaulika" na nchi za Magharibi. Kufuatia hali hii, CPC kilisema wazi kwamba kinapinga nchi za magharibi kuingilia masuala ya ndani ya Afrika na kuunga mkono nchi za Afrika kuchagua mifumo ya kisiasa na maendeleo kulingana na hali zao za kitaifa. Pendekezo hili lilipokelewa na kupongezwa na watu wa nchi za Afrika. Wakati CPC kikiiunga mkono Afrika kimataifa, pia kimeimarisha ushirikiano wa kunufaishana na nchi za Afrika. Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC lilianzishwa rasmi mwaka 2000, likizindua njia ya kuheshimiana na ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi zinazoendelea.

 

Tangu kuanzishwa kwa FOCAC, thamani ya biashara kati ya China na Afrika na uwekezaji wa China barani Afrika umeongezeka kwa mara 28 na mara 100 mtawalia, na mchango uliotolewa na China kwa ukuaji wa uchumi wa Afrika umezidi 20% kwa miaka mingi. “Bara la matumaini" na "ardhi ya maendeleo"... Kuinuka kwa Afrika imekuwa mada motomoto katika jumuiya ya kimataifa. Baada ya China na Afrika kuungana mikono katika kupambana na janga la COVID-19 na kuonyesha udugu wa China na Afrika wa kushirikiana kwa vitendo, kauli ya Xi Jinping ya kwamba "China na Afrika zimekuwa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja tangu zamani" imefanya matokeo ya ushirikiano wa kirafiki kati ya watu wa China na Afrika "yaonekane na kupatikana zaidi”.

 

Ripoti ya kazi ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC imesema, “China inaimarisha mshikamano na ushirikiano na nchi zinazoendelea, na kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea.” Inaaminika kuwa katika mchakato wa China kujiendeleza kisasa, CPC kitaendelea kuiongoza China ya kisasa inayochangamkia kunufaika na fursa za maendeleo za nchi za Afrika, na kufanya ndoto za China na Afrika zisaidiane.