Maonyesho ya Tatu ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika yafunguliwa mjini Changsha
2023-06-30 08:39:16| cri

Maonesho ya Tatu ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika yamefunguliwa jana Alhamis huko Changsha, China.

Kaulimbiu ya maonyesho hayo ni "Kutafuta maendeleo ya pamoja na mustakabali wa kunufaishana kwa pamoja". Nchi za Benin, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Madagascar, Malawi, Morocco, Msumbiji, Nigeria, na Zambia zimekuwa nchi za heshima katika maonyesho hayo.

Maonyesho hayo yamevutia waonyeshaji 1,500, ikiwa ni ongezeko la asilimia 70 ikilinganishwa na kipindi kilichopita. Bidhaa 1,590 kutoka nchi 29 zilionyeshwa katika maonyesho hayo, ikiwa ni ongezeko la asilimia 165.9 kuliko maonesho hayo yaliyopita.