Wanariadha wa Kenya Robert Kipkemboi na Naomi Jebet, wamepata ushindi kwenye mbio za marathon za Mji wa Nairobi katika mazingira ya ukungu na baridi.
Ushindi huo umempatia kila mmoja kitita cha karibu dola elfu 25 za kimarekani, kwenye mbio zilizoanzia kwenye eneo la Elgeyo Marakwet huku sehemu kubwa ya mbio hizo ikiwa ni kwenye barabara kuu ya Nairobi.
Kipkemboi mwenye umri wa miaka 33 ametumia muda wa saa 2:07:38, Jebet ametumia muda wa saa 2:25:33.
Hata hivyo wanariadha wa Kenya hawakufua dafu kwenye mbio za nusu marathon baada ya Maxwell Rotich wa Uganda kupata ushindi kwa muda wa saa 1:00:10 akiwashinda Vincent Kipkorir na Kennedy Kimutai.