Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania yatoa tahadhari kuhusu upepo mkali na mawimbi makubwa
2023-07-03 08:35:03| CRI

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania TMA imetoa tahadhari kuhusu upepo mkali na mawimbi makubwa yanayoweza kutokea kwenye maeneo ya pwani.

Kwenye taarifa yake mamlaka hiyo imesema upepo mkali wenye kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa ya bahari yanayoweza kufikia urefu wa mita mbili yanakadiriwa kuyakumba maeneo ya pwani ya bahari ya Hindi.

Kwa mujibu wa TMA, maeneo yatakayoathirika ni mikoa ya Lindi, Mtwara, Tanga, Dar es Salaam, Pwani, pamoja na visiwa vya Zanzibar.