Maonyesho ya tatu ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika yamekuwa na ushiriki mkubwa zaidi
2023-07-03 10:50:32| CRI

Maonyesho ya tatu ya uchumi na biashara ya China na Afrika yalimalizika jana jumapili, na miradi 120 yenye thamani ya jumla ya dola za kimarekani bilioni 10.3 ilisainiwa.

Maonesho hayo ya siku nne yalianza Alhamisi huko Changsha, Mkoani Hunan katikati mwa China. Hunan ni moja ya mikoa inayofanya juhudi zaidi katika kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na Afrika.

Naibu katibu mkuu wa serikali ya mkoa wa Hunan Bw. Zhou Yixiang amesema wageni 1,700 kutoka nje na wengine zaidi elfu 10,000 wa ndani, walishiriki kwenye maonyesho ya mwaka huu na ushiriki huo ulikuwa wa kiwango cha juu zaidi kuliko awamu zilizopita.

Maonesho hayo yamedhihirisha uhai na ustahimilivu mkubwa wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika.