UM na UA wapongeza wanajeshi wa Burundi kwa kulinda usalama wa Somalia
2023-07-03 09:14:27| CRI

Wajumbe wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa nchini Somalia wamewapongeza walinzi wa amani wa Burundi kwa juhudi zao za kulinda utulivu nchini Somalia.

Mjumbe maalumu wa Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia Bw. Mohammed El-Amine Souef amesema Burundi imetoa mchango mkubwa katika suala la amani kwa wote kwa kutumia njia ya kisiasa zikiwemo upatanishi na ushiriki endelevu kwenye shughuli hiyo.

Naibu mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa UM na mkuu wa tume ya Umoja wa mataifa ya kutoa msaada nchini Somalia Bi. Anita Kiki Gbeho amewapongeza walinda amani hao kwa ushujaa na kujitolea kwao na pia ameahidi kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono juhudi za Tume ya Umoja wa Afrika nchini humo.