Kenya yaondoa marufuku ya miaka sita ya ukataji miti na kuzusha malalamiko kutoka wanamazingira
2023-07-04 09:04:07| CRI

Serikali ya Kenya imeondoa marufuku ya miaka sita ya ukataji miti katika misitu ya taifa licha ya wasiwasi wa wanaharakati wa mazingira.

Idara ya Misitu ya Kenya (KFS) imesema jamii zinazopakana na misitu hiyo zitanufaika kutokana na uvunaji wa miti uliopangwa, jambo hilo limelalamikiwa na wanamazingira wa Kenya, kwani uamuzi huo umekuja wakati Kenya inakabiliwa na athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabia nchi.

Jumapili iliyopita Rais William Ruto alitangaza kuondolewa kwa marufuku ya ukataji miti, akisema kuna haja ya kuyafungua kiuchumi maeneo yanayotegemea misitu, na kwamba serikali yake imeweka mikakati ya kuhakikisha miti iliyokomaa tu ndiyo inayovunwa, na huku mingine ikipandwa.