Mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu wa Jukwaa la Hatua za Dunia kwa ajili ya Maendeleo ya Pamoja kufanyika Beijing
2023-07-04 08:50:02| CRI

Msemaji wa Shirika la Taifa la Ushirikiano wa Maendeleo wa Kimataifa la China Bw. Xu Wei, amesema mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu wa Jukwaa la Hatua za Dunia kwa ajili ya Maendeleo ya Pamoja utafanyika hapa Beijing kuanzia tarehe 9 hadi 10 Julai. Wajumbe kutoka nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 130 watahudhuria au kushiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao.

Mwezi Septemba mwaka 2021, Rais Xi Jinping alitoa Pendekezo la Maendeleo Duniani kwenye kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Mwezi Juni mwaka jana, Rais Xi alitangaza hatua 32 za kiutendaji za kutekeleza pendekezo hilo, kufanyika kwa mkutano huo kukiwa ni moja ya hatua hizo.