Mamlaka ya Maendeleo ya Kiserikali (IGAD), imezindua mpango maalumu kuhimiza mawasiliano ya watu kati ya Ethiopia na Djibouti.
Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, pendekezo hilo linaloitwa “Mpango wa Treni ya IGAD kwa Ushirikiano wa Kikanda” ni ushirikiano wa pamoja kati ya Ethiopia na Djibouti chini ya uongozi wa IGAD, ukiashiria hatua kubwa kuelekea kuhimiza mafungamano ya kikanda na kuimarisha urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Katibu mtendaji wa IGAD Bw. Workneh Gebeyehu amesema kwenye hafla ya uzinduzi kuwa Ethiopia inaungana na Djibouti kwa njia ya ardhi na inategemea bandari za Djibouti kuagiza na kuuza bidhaa nje, na asilimia 95 ya biashara zake zinapita kwenye nchi hiyo.
Ameongeza kuwa kuunganishwa miundombinu muhimu ikiwemo ya uchukuzi, mawasiliano ya simu, biashara na uwekezaji, usalama, nishati ya umeme na maliasili ya maji, kumeimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.