Palestina yatangaza kusimamisha mawasiliano na mkutano wowote na Israel
2023-07-04 09:41:47| CRI

Palestina imetangaza kusimamisha mawasiliano na mkutano wowote na Israel, ili kupinga mauaji ya wapalestina 8 yaliyofanywa na jeshi la Israel huko Jenin katika ukingo wa magharibi wa mto Jordon.

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina ametoa uamuzi huo kwenye mkutano wa dharura wa viongozi wa Palestina huko Ramallah. Uamuzi huo pia ni pamoja na kuendelea kusimamisha uratibu wa kiusalama na upande wa Israel. Rais Abbas pia ametoa mwito kwa makundi mbalimbali ya Palestina kuitisha mikutano na kujadili hali ya wasiwasi kwenye eneo la Jenin.

Jeshi la Israel jana alfajiri lilifanya mashambulizi huko Jenin na kusababisha vifo vya watu 8 na wengine zaidi 80 kujeruhiwa.