Rais Xi Jinping asisitiza kipaumbele kwa usalama na mali za wananchi katika kukabiliana na maafa
2023-07-05 08:44:05| CRI

Rais Xi Jinping wa China ameagiza mamlaka katika ngazi zote kutoa kipaumbele katika kuhakikisha usalama na mali za wananchi, na kujitahidi kupunguza hasara katika kazi ya kukabiliana na mafuriko na maafa mengine.

Rais Xi ametoa kauli hiyo kwenye agizo muhimu baada ya mvua kubwa za mfululizo kuyakumba maeneo mbalimbali ikiwemo mji wa Chongqing, na kusababisha vifo vya watu na hasara ya mali.

Rais Xi ameagiza Makao Makuu ya Udhibiti wa Mafuriko na Ukame na Wizara za Usimamizi wa Dharura na Raslimali za Maji kuongeza uratibu, kuimarisha utafiti na kuboresha utoaji wa tahadhari za mapema na utabiri.

Rais pia amesisitiza kuwa maofisa viongozi katika ngazi zote wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na mafuriko, kutoa kipaumbele kwa usalama wa wananchi na mali zao, na kujitahidi kupunguza madhara ya aina zote.