Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia uratibu wa mambo ya kibinadamu UNOCHA imetoa taarifa mpya ikisema, idadi ya watu walioingia Ethiopia kutoka Sudan inakaribia elfu 60.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo hadi kufikia Juni 28, watu zaidi ya elfu 57 wameingia Ethiopia kupitia vituo vya mpakani Metema na Kurmuk kati ya Ethiopia na Sudan.
Ofisi hiyo imesema idadi ya wastani ya watu wanaowasili huko Metema kwa siku imefikia 500 hadi 1,000, siku kadhaa zilizopita zimeonesha ongezeko katika idadi ya raia wa Sudan wanaowasili, ambayo imezidi idadi ya raia wa Ethiopia waliorudi ikifuatiwa na raia wa nchi ya upande wa tatu.