China yasikitishwa na ripoti ya IAEA kuhusu mpango wa Japan wa kutoa maji ya nyukilia baharini
2023-07-05 22:43:21| cri

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limetoa ripoti ya kutathmini kazi ya Japan kushughulikia maji taka ya nyuklia, na kuona mpango wake wa kutoa maji hayo baharini unalingana na vigezo vya kimataifa vya usalama. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema ripoti hiyo haioneshi vya kutosha wataalam walioshiriki kwenye kazi ya kutathmini, na pia haikubaliwi na wataalam wote, China inasikitishwa na ripoti hiyo.

Msemaji huyo ameihimiza tena Japan kuacha mpango wa kutoa maji taka ya nyuklia baharini, na kuyashughulikia kwa njia wazi ya kisayansi na kiusalama. Pia amesema China inaitaka Japan ishirikiane na IAEA kuanzisha kwa haraka utaratibu wa kimataifa wa muda mrefu wa uchunguzi utakaoshirikisha pande mbalimbali husika zikiwemo nchi zake jirani.