Serikali ya Somalia imethibitisha kuwa imechukua majukumu ya usalama kutoka kwa askari 2,000 wa Tume ya Umoja wa Afrika nchini humo ATMIS katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo.
Wizara ya ulinzi wa taifa ya nchi hiyo imesema kikosi cha usalama cha Somalia kimemaliza kipindi cha kwanza cha Tume ya ATMIS kupunguza kikosi katika sekta tano kulingana na maazimio nambari 2628 na 2670 ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikiwa ni hatua muhimu kwenye mchakato wa kuleta utulivu nchini humo.
Hadi kufikia Juni 30 tume ya ATMIS imekabidhi vituo sita vya kijeshi kwa kikosi cha usalama cha Somalia, ikiashiria hatua muhimu kwa nchi hiyo kuelekea kujitegemea katika usalama.