Mkutano wa 23 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai(SCO) ulifanyika jana, na kutoa maazimio mawili muhimu.
Azimio la kwanza linahusu ushirikiano wa kupambana na siasa kali zinazochochea ugaidi, ufarakanishaji na itikadi kali, ikisisitiza nchi wanachama kuimarisha ushirikiano na uratibu wa pande zote katika viwango vya kitaifa, kikanda na dunia nzima ili kukabiliana changamoto za kiusalama.
Azimio la pili linahusu ushirikiano katika mageuzi ya kidigitali, ambayo imeeleza kuwa nchi wanachama zinatakiwa kushirikiana katika kuhimiza ukuaji wa mambo ya kidigitali katika sekta mbalimbali ili kuwanufaisha raia wao.
Licha ya maazimio hayo mawili, mkutano huo pia umepitisha ombi la Iran kuwa nchi mwanachama rasmi wa SCO, na kufanya idadi ya nchi wanachama wa jumuiya hiyo ifikie 9.