Rais Xi Jinping wa China atoa salamu za pole kwa mwenzake wa Kenya kufuatia kutokea kwa ajali kubwa ya barabarani
2023-07-05 09:26:45| CRI

Rais Xi Jinping wa China tarehe 3 alitoa salamu za pole kwa mwenzake wa Kenya William Samoei Ruto kufuatia ajali kubwa ya barabarani kutokea nchini humo. Rais Xi ametoa salamu za rambirambi kwa wafiwa na pole kwa majeruhi katika ajali hiyo iliyotokea Julai 1 katika kaunti ya Kericho, magharibi mwa Kenya.