Botswana yataka kuuza nyama ya ng’ombe kwa China haraka iwezekanavyo
2023-07-05 09:34:51| CRI

Waziri wa kilimo wa Botswana Fidelis Molao, amesema Botswana inatarajia kuuza nyama bora ya ng’ombe kwa China haraka iwezekanavyo.

Akiongea nchini Botswana baada ya kurudi kutoka mjini Changsha, Hunan nchini China alikohudhuria Maonesho ya awamu ya tatu ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika, Bw. Molao amesema nchi hiyo inafanya juhudi na kutarajia kusaini makubaliano na China ili kuingia kwenye soko la nyama ya ng’ombe la China.

Ameongeza kuwa nchi hiyo pia inatarajia kuingia kwenye sekta ya mauzo ya bidhaa za machungwa kwa nchi za nje kuanzia mwaka 2025.