Ripoti ya IAEA haiwezi kuthibitisha usalama wa mpango wa Japan kumwaga maji taka ya nyukilia baharini
2023-07-06 15:22:44| cri

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) hivi karibuni lilitoa ripoti kuhusu mpango wa Japan wa kumwaga maji taka ya nyukilia baharini, ambayo inachukuliwa na Japan kama ushahidi wa usalama wa mpango huo. Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limetoa tahariri, na kusema ripoti ya IAEA haiwezi kuthibitisha usalama wa mpango wa Japan kumwaga majitaka ya nyukilia baharini.

Tahariri hiyo inasema majukumu ya IAEA ni kuhimiza matumizi ya teknolojia ya nyukilia kwa usalama na amani, sio kutathmini athari ya maji taka ya nyukilia kwa mazingira ya bahari na usalama wa viumbe. Sampuli na data zote zilizopatikana na shirika hilo zimetolewa na Japan, lakini Kampuni ya Umeme ya Tokyo inayomiliki Kiwanda cha Umeme wa Nyukilia cha Fukushima imekuwa ikisema uwongo mara nyingi katika suala hili. Habari zilizotolewa na vyombo vya habari vya Korea Kusini zinasema kabla ya IAEA kutangaza ripoti hiyo, serikali ya Japan iliipata na kuisahihisha. Ili kufanya hivyo, Japan ilitoa Euro zaidi ya milioni moja kwa wafanyakazi wa IAEA. 

Tahariri hiyo inaona kuwa bila kujali ripoti hiyo imesema nini, mpango wa Japan kumwaga maji taka ya nyukilia baharini katika miaka 30 ijayo hauruhusiwi, kwani utaathiri binadamu wote.