Rais wa China ampongeza Julius Maada Bio kwa kuchaguliwa tena kuwa rais wa Sierra Leone
2023-07-06 16:32:52| cri

Rais Xi Jinping wa China amempongeza Julius Maada Bio kwa kuchanguliwa tena kuwa rais wa Sierra Leone.

Rais Xi amesema urafiki kati ya China na Sierra Leone una historia ndefu, na katika miaka ya hivi karibuni, nchi hizo mbili zimezidi kuaminiana kisiasa, kudumisha ushirikiano wenye mafanikio makubwa, na kushirikiana vizuri katika mambo ya kimataifa.

Amesisitiza kuwa anatilia maanani sana kuendeleza uhusiano kati ya China na Sierra Leone, na kupenda kushirikiana na rais Bio kuungana mkono, kushikamana na kushirikiana, ili kuhimiza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati katika pande zote kati ya nchi hizo mbili kupata maendeleo ya mfululizo, na kunufaisha zaidi wananchi wao.