Waziri Mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa jana alipongeza ushiriki wa waonyeshaji zaidi 100 wa China katika maonyesho ya 47 ya biashara ya Dar es Salaam (DITF), ambayo ni jukwaa la kukuza biashara ya kimataifa katika eneo ya Afrika Mashariki na Kati.
Akizindua maonyesho hayo yatakayofanyika hadi tarehe 13, Bw. Majaliwa amesema idadi kubwa ya washiriki wa China kwenye maonesho hayo ni ushuhuda wa uhusiano mzuri wa kibiashara kati ya China na Tanzania.
Bw. Majaliwa amesema maonyesho ya biashara ya mwaka huu yamevutia waonyeshaji wa ndani 3,384 na washiriki wa nje kutoka nchi 16.
Pia amemshukuru mfadhili mkuu wa maonesho hayo, Kituo cha Biashara na Ugavi cha Afrika Mashariki, na wafadhili wengine kwa kufanikisha maonyesho hayo.