Waziri wa hazina ya taifa na mipango ya uchumi wa Kenya Bw. Njuguna Ndung'u amesema serikali imeweka lengo la mfumuko wa bei kuwa asilimia 5 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ili kudumisha utulivu wa uchumi.
Bw. Ndung'u amesema lengo hilo litakuwa na ukomo wa unyumbufu wa asilimia 2.5. Amesema kiwango hicho kina lengo la kukabiliana na athari za mitikisiko ya nje kama vile mgogoro wa Ukraine na Russia na changamoto nyingine za dunia kwa uchumi wa Kenya.
Ili kudhibiti ongezeko la mfumuko wa bei, Benki Kuu ya Kenya mwishoni mwa mwezi Juni iliongeza kiwango cha mikopo kwa asilimia 1 hadi asilimia 10.5, likiwa ni ongezeko kubwa zaidi tangu 2018.