Rais wa China afanya ziara ya ukaguzi mkoani Jiangsu
2023-07-06 21:29:16| CRI

Rais Xi Jinping wa China amefanya ziara ya ukaguzi mkoani Jiangsu kuanzia tarehe 5 hadi 6 mwezi huu.

Jumatano mchana, rais Xi alikagua mji wa Suzhou, na kutembea Kituo cha Maonesho ya Eneo la Viwanda la Suzhou, ili kupata ufahamu kuhusu ujenzi wa eneo la sayansi na teknolojia za hali ya juu. Eneo hili limeshika nafasi ya kwanza katika tathmini kamili ya maeneo ya kitaifa ya maendeleo ya uchumi kwa miaka saba mfululizo, na linajitahidi kujengwa kuwa eneo la teknolojia ya juu duniani.

Siku hiyo hiyo rais Xi pia alitembelea Kampuni ya Sayansi na Teknolojia ya Huaxing Yuanchuang ya Suzhou, ili kupata ufahamu kuhusu uendeshaji wa kampuni hiyo inayotengeneza vifaa vya semiconductor, na mapato yake ya mwaka 2022 yamezidi yuan bilioni 2, sawa na dola za kimarekani milioni 274.

Leo asubuhi, rais Xi alitembelea mtaa wa kihistoria na kitamaduni wa Pingjiang, ili kukagua hali ya uhifadhi wa mtaa huo maarufu wenye historia ndefu.