Xi aitaka Jiangsu kuongoza katika kuendeleza China ya kisasa
2023-07-07 15:56:48| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametoa wito kwa mkoa wa Jiangsu nchini humo kuwa mbele na kuwa mfano wa kuigwa katika kuendeleza China ya kisasa.

Rais Xi ametoa wito huo katika ziara ya ukaguzi huko Jiangsu aliyofanya kuanzia Jumatano hadi Ijumaa. Akisifu nguvu za msingi imara wa viwanda wa Jiangsu, rasilimali nyingi za kisayansi na kielimu, mazingira mazuri ya biashara na ukubwa wa soko, Xi aliutaka mkoa huo kuendelea na jukumu la kupigiwa mfano katika kukuza mageuzi, uvumbuzi na maendeleo ya hali ya juu, pamoja na kuchangia juhudi za China katika kukuza mwelekeo mpya wa maendeleo.

Katika ziara yake, Xi alitembelea miji ya Suzhou na Nanjing, na kwenda sehemu zikiwemo bustani ya viwanda, kwenye makampuni, jengo la kihistoria na kitamaduni, na maabara ya sayansi.