Rais wa CAR afanya ziara ya kikazi nchini Kongo
2023-07-10 08:48:46| CRI

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) Faustin-Archange Touadera aliwasili Jumapili asubuhi huko Oyo, kaskazini mwa Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Kongo.

Rais Touadera, ambaye yuko katika ziara ya kikazi, alilakiwa katika uwanja wa ndege wa Ollombo na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kongo Raymond Zephiryn Mboulou. Katika ziara yake, rais wa Kongo atakuwa na mazungumzo naye kuhusu ushirikiano kati ya Kongo na Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambazo zote ni nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi na Kifedha ya Afrika ya Kati (CEMAC).

Ziara ya Rais Touadera inaambatana na ile ya Rais wa Kenya William Ruto, ambaye alikaribishwa mjini Oyo Jumamosi alasiri na rais wa Kongo. Marais hao watatu walikutana kujadili mada zinazohusiana na mabadiliko ya tabia nchi, usalama na maendeleo barani Afrika. Rais Ruto na ujumbe wake wameondoka Oyo Jumapili kuelekea Nairobi, Kenya.