Waziri wa ulinzi wa Somalia Abdulkadir Mohamed Nur alisema wapiganaji 40 wa kundi la al-Shabab waliuawa jana Jumapili na vikosi vya jeshi la Somalia maarufu kama Danab, kwenye operesheni ya pamoja na vikosi vya kikanda na kimataifa iliyofanyika katika eneo la lower Juba, kusini mwa Somalia.
Nur alisema shambulizi la vikosi vya pamoja limefanikiwa kuzuia wapiganaji wa al-Shabab, ambao wanajipanga upya kwa ajili ya maandalizi ya kushambulia maeneo waliyoyalenga.
Nur hakutaja kama kuna vifo na majeruhi kwa upande wa jeshi au la, ambalo limeimarisha mashambulizi ya anga na operesheni za ardhini dhidi ya wapiganaji hao wenye uhusiano na kundi la al-Qaeda kwenye ngome zao zilizoko katikati na kusini mwa Somalia.