Kampuni ya Wondfo Biotech ya China yazindua kituo cha pamoja cha mafunzo ya maabara na chuo kikuu cha Kenya
2023-07-11 08:58:30| CRI

Kampuni Wondfo Biotech ya Guangzhou, ambayo ni kampuni inayotengeza na kusambaza vifaa vya uchunguzi ya China, imezindua kituo cha mafunzo ya maabara kwa pamoja na kitivo cha sayansi ya afya katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya. Kituo hicho ni kwa ajili ya kuongeza huduma za upimaji wa magonjwa ya kuambukiza na ya mtindo wa maisha nchini humo.

Mkurugenzi wa Wondfo Biotech wa Kenya Bw. Xiong Bear amesema kuanzishwa kwa kituo hicho kutaboresha uwezo wa wanafunzi wanaosomea mambo ya afya na wahadhiri wao kuendesha vifaa vya uchunguzi.

Mkuu wa kitivo cha sayansi ya afya katika Chuo Kikuu cha Nairobi George Osanjo amesema kuanzishwa kwa kituo cha mafunzo ya maabara ni hatua muhimu katika ushirikiano kati ya China na Kenya katika uwanja wa matibabu. Amebainisha kuwa kituo hicho pia kinaendana na maono yao ya kuimarisha uhusiano kati ya chuo na sekta hiyo.