Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani shambulio dhidi ya tume ya ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
2023-07-12 19:11:26| cri

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeaani vikali shambulio dhidi ya Tume ya Kulinda Amani ya Umoja huo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati lililotokea jumatatu na kusababisha kifo cha mlinda amani kutoka nchini Rwanda.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, nchi wajumbe wa Baraza hilo wametoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na kwa serikali ya Rwanda na kwa Umoja wa Mataifa. Pia wameitaka serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati kufanya uchunguzi wa shambulio hilo kwa kushirikiana na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo, ili kuwafikisha washukiwa wa shambulio hilo mbele ya sheria.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa taarifa akilaani vikali shambulio hilo, na kuzitaka mamlaka za nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kutumia juhudi zote kuwatambua washukiwa wa shambulio hilo na kuwafikisha mbele ya sheria haraka iwezekanavyo.