Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Maeneo Kame nchini Kenya Rebecca Miano amesisitiza umuhimu wa sekta binafsi katika kuboresha ukuaji wa uchumi kwenye ngazi za kitaifa, kikanda na bara zima la Afrika.
Katika taarifa iliyotolewa na Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mjini Arusha Tanzania imesema, Bi. Miano amesema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa Jukwaa la 14 la Ngazi ya Juu ya Umoja wa Afrika kuhusu Sekta Binafsi lililofanyika mjini Nairobi.
Amesema sekta binafsi inachukua asilimia 80 ya uzalishaji wa jumla barani Afrika, moja ya tatu ya uwekezaji, na robo tatu ya faida, na pia kutoa ajira kwa asilimia 90 ya idadi ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi barani Afrika. Pia amesema, sekta binafsi iliyo imara ni muhimu sana katika kutimiza mageuzi endelevu ya kiuchumi barani Afrika.