Xi Jinping aongoza mkutano wa pili wa kamisheni ya kuimarisha mageuzi ya kamati kuu ya CPC
2023-07-13 15:08:02| cri

Katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Rais wa China na mkurugenzi wa kamisheni ya kuimarisha mageuzi iliyo chini ya Kamati Kuu ya CPC, Xi Jinping, Jumanne alasiri aliongoza mkutano wa pili wa kamisheni hiyo, na kupitisha Mwongozo Kuhusu Kujenga Mfumo Mpya wa Uchumi Unaofungua Mlango kwa Kiwango cha Juu Zaidi na Kuhimiza Uundaji wa Muundo Mpya wa Maendeleo.

Xi Jinping amesisitiza kuwa, kujenga mfumo mpya wa uchumi unaofungua mlango kwa kiwango cha juu zaidi ni hatua ya kimkakati ya kuboresha maendeleo na mageuzi kupitia ufunguaji mlango, na inatakiwa kutilia mkazo katika kuhudumia uundaji wa muundo mpya wa maendeleo na kuendeleza ufunguaji mlango wa kimfumo. Pia kuimarisha mageuzi ya kimfumo kwa kutoa kipaumbele katika nyanja muhimu za ushirikiano na mataifa ya nje ikiwemo uwekezaji, biashara, fedha na uvumbuzi, na kukamilisha sera na hatua zinazohusika, ili kuinua ufunguaji mlango wa China hadi kufikia kwenye kiwango kipya.