Wanaharakati wa Afrika wasema mahitaji yanayoongezeka ya protini zinazotokana na wanyama yanachochea mgogoro wa tabianchi
2023-07-13 22:08:59| cri

Wanaharakati wa Afrika wamesema, mahitaji yanayoongezeka ya protini zinaotokana na wanyama, ikiwemo nyama ya ng’ombe, nguruwe, kondoo, mayai na maziwa, yanachochea mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi barani Afrika kupitia utoaji wa methane.

Akizungumza kwenye Mkutano wa pili wa Kilele wa Protini barani Afrika uliofanyika jijini Nairobi, Kenya, Mkurugenzi wa Afrika katika Shirika la Kimataifa la Ulinzi wa Wanyama (WAP) Bw. Tennyson Williams amesema, uzalishaji wa protini hizo zinazotokana na wanyama ili kukabiliana na mahitaji makubwa katika miji ya Afrika pia umesababisha kukatwa kwa misitu, upotevu wa viumbe hai, na kulifanya bara hilo kukabiliwa na hali mbaya ya hewa.

Naye meneja kampeni wa WAP Victor Yamo amesema, ulaji wa nyama barani Afrika unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 30 itakapofika mwaka 2030, hivyo kulazimu uzalishaji wa wanyama viwandani, hatua inayoathiri mfumo wa ikolojia na afya ya binadamu.