Tume ya Mpito ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) na Ofisi ya Msaada ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia (UNSOS) zinatoa mafunzo kwa wanajeshi na askari polisi 55 kuhusu usambazaji wa ufanisi na ufikishaji wa mafuta katika mazingira mazuri kwenye maeneo ya vita na yenye machafuko.
Tume ya Umoja wa Afrika imesema katika taarifa yake iliyotolewa mjini Mogadishu, kuwa kuboreshwa kwa mnyororo wa ugavi wa mafuta ni sehemu muhimu katika kuhakikisha mafanikio ya operesheni ya pamoja dhidi ya wapiganaji wa kundi la al-Shabab.
Mafunzo hayo yaliyoanza jumanne na yanatarajiwa kumalizika kesho Ijumaa, yanalenga kuhakikisha upatikanaji endelevu, wa kutosha na kwa wakati wa petrol, mafuta na mafuta ya kulainisha katika njia ambayo ni rafiki wa mazingira.