Ghasia zaibuka polisi Kenya wakikabiliana na waandamanaji
2023-07-13 21:09:59| cri

Vurugu zimezuka katika viwanja vya Kamukunji jijini Nairobi, Kenya, baada ya askari polisi wa kupambana na ghasia kuwatawanya waandamanaji wa upinzani waliofika kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya mkutano ulioitishwa na viongozi wa muungano wa Azimio la Umoja.

Maofisa hao walivamia uwanjani hapo na kuanza kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya vijana waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo kwa ajili ya maandamano dhidi ya serikali ya Rais William Ruto.

Jumanne wiki hii, Rais Ruto alinukuliwa akisema kwamba hataruhusu maandamano kuendelea nchini humo akisema watu sita waliuawa kufuatia maandamano hayo Ijumaa iliyopita.