Rais wa Msumbiji asema uwekezaji katika afya utahakikisha maendeleo jumuishi
2023-07-14 22:42:04| cri

Rais wa Msumbiji Felipe Nyusi amesema, uwekezaji katika sekta ya afya utahakikisha hatma ya sasa na ya baadaye ya taifa hilo, na pia kusaidia ujumuishi wa jamii.

Rais Nyusi amesema hayo katika ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Miundombinu ya Afya, uliofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo, Maputo, na kuhudhuriwa na Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dr. Tedros Ghebreyesus.

Katika hotuba yake, rais Nyusi amesema uwekezaji katika sekta ya afya ni kupambana na umasikini na ukosefu wa usawa wa kiuchumi na kijamii, na kwamba ni muhimu kwa wenzi wa kitaifa na kimataifa kutenga rasilimali katika sekta ya afya ili kuhakikisha jamii yenye afya na uwezo wa kuchangia katika maendeleo ya nchi.

Kwa upande wake, Dr. Ghebreyesus amesema, Msumbiji itapokea dozi za chanjo dhidi ya Malaria katika nusu ya pili ya mwaka ujao.

Kwa sasa, Msumbiji imewekeza karibu dola za kimarekani 30 katika huduma ya afya kwa kila raia wake.