Wang Yi aitaka Marekani kuchukua hatua madhubuti kurejesha uhusiano kati ya China na Marekani kwenye njia sahihi
2023-07-14 08:58:38| CRI

Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Wang Yi amesema kwamba Marekani inapaswa kuchukua hatua madhubuti ili kuufanya uhusiano kati ya China na Marekani urudi kwenye njia sahihi.

Bw. Wang amesema hayo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, kando ya mikutano ya mawaziri wa mambo ya nje wa ASEAN, akisistiza kuwa pande zote mbili zimefikia makubaliano kupitia mawasiliano ya kina na ya wazi, wakati wa ziara ya Blinken nchini China mwezi uliopita.

Ametoa wito kwa Marekani kuwa na mtazamo wa busara na kiutendaji na kushirikiana na China na kuwa na mwelekeo mmoja ili kuendeleza mashauriano kuhusu kanuni elekezi za China na Marekani, kupanua njia za mawasiliano ya kidiplomasia na kiusalama, kuboresha ufanisi wa mawasiliano, na kurahisisha mawasiliano kati ya watu wa nchi hizo mbili.