Tanzania yasherehekea maadhimisho ya miaka 96 ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China
2023-07-14 09:05:49| CRI

Serikali ya Tanzania Jumatano jioni iliipongeza China kwa kuadhimisha miaka 96 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA), ambayo yatafanyika Agosti 1.

Akizungumza katika sherehe za kuadhimisha miaka 96 ya PLA zilizofanyika katika Ubalozi wa China jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Tanzania Innocent Bashungwa, alisema maadhimisho haya ni kielelezo cha safari ndefu yenye mafanikio ambayo PLA imepitia na kutoa mchango mkubwa katika sekta za ulinzi nchini China, na nje ya China. Bashungwa pia aliishukuru China kwa msaada wake thabiti katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania, ikiwa ni pamoja na katika sekta ya ulinzi na usalama.

Naye Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema tangu kuundwa kwake na Chama cha Kikomunisti cha China Agosti 1, 1927, PLA limekuwa na nguvu isiyoyumba katika kuleta uhuru na ukombozi wa taifa la China, kulinda mamlaka ya taifa ya China na ukamilifu wake wa ardhi, ustawi wa nchi, na kukuza ustawi wa watu wa China.

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), viongozi wa serikali na wawakilishi kutoka nje ya nchi walipo Tanzania.