China yalaani vikali tukio la kuchoma Qur’an
2023-07-14 08:59:48| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Wang Wenbin Alhamisi alisema China inalaani vikali tukio la kuchoma Qur’an lililotokea tena katika nchi husika, akiongeza kuwa ule unaoitwa “uhuru wa kujieleza” usiwe sababu ya kuchochea migogoro na uadui kati ya ustaarabu.

Kuanzia tarehe 11 hadi 12 Julai, mkutano wa 53 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ulifanya mjadala wa dharura juu ya tukio la kuchoma Qur’an katika nchi husika, na kupitisha rasimu ya azimio lililopendekezwa na Shirika la Ushirikiano wa Kiislamu kwa kura 28 za ndiyo, kura 12 za hapana na kura 7 zisizopigwa. Azimio hilo linalaani tukio la hivi karibuni la kuikufuru Qur’an hadharani, na kuamua kufanya warsha na mazungumzo kwenye mkutano wa 54 na 55 wa Baraza la Haki za Binadamu, na kumwalika Kamishna Mkuu kuwasilisha taarifa mpya juu ya chanzo cha chuki za kidini.

Msemaji huyu alisema China inaunga mkono kufanyika kwa mjadala huo wa dharura, na kulaani tukio hilo la kuchoma Qur’an. China pia inatetea kuheshimiana na kujumuishana na kufundishana kati ya ustaarabu, na kupinga kithabiti chuki za aina yoyote dhidi ya Uislamu.