Hivi karibuni baadhi ya nchi zinazoendelea zimekumbwa na hatari inayoongezeka ya kushindwa kulipa madeni yao kutokana na sababu mbalimbali, na nchi za magharibi zimetumia fursa hii kusambaza nadharia yao potofu inayodai kuwa“Ukanda Mmoja, Njia Moja” ndio ni chanzo cha“mtego wa madeni”. Lakini ukweli ni kwamba, hakuna mshirika yeyote wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” anayekubali shutuma hiyo.
Akizungumzia suala hilo, msomi wa Nigeria Dkt. Michael Ehizuelen amesema, yaliyoletwa na mpango wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” sio “mtego wa madeni”, bali ni chachu kwa maendeleo ya uchumi.
Akihojiwa hivi karibuni na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, Dkt. Ehizuelen anaona kuwa, kupitia utekelezaji wa pamoja wa Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, China na nchi zilizoko katika “Ukanda Moja, Njia Moja” zinajenga dunia inayofungamana. Mpango wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” si kama tu umesukuma mbele maendeleo ya miundombinu na uchumi, na bali pia umehimiza ushirikiano wa kiutamaduni na kiafya, na hivyo kuzidisha maslahi ya umma. Msomi huyo anaona kuwa hii ni tofauti kabisa na hatua zilizochukuliwa na nchi za magharibi. Amesema, nchi za magharibi siku zote zinahofia kupoteza udhibiti kamili wa dunia, kwa kuwa zimekuwa zikiiba au kupora rasilimali kutoka dunia nzima hasa Afrika ili kutimiza maendeleo yao yenyewe. Lakini pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” linalenga kuhimiza maendeleo na ustawi wa pamoja, lengo ambalo ni tofauti kabisa na ubeberu na ukoloni wa nchi za magharibi. China inatarajia kuijenga Afrika na dunia iliyo bora zaidi, na China inaona kuwa ustawi wa uchumi wa dunia pia una manufaa kwa maendeleo yake yenyewe.
Akitolea mfano, Dkt. Ehizuelen amesema ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” umeboresha miundombinu katika nchi za Afrika Mashariki, kuhimiza ukuaji wa biashara na kuleta manufaa ya kiuchumi, na ni kutokana na mpango huo, nchi za Afrika Mashariki zinageuza utajiri wao wa rasilimali kuwa msukumo wa maendeleo halisi. Kwa upande wa madeni, katika mkutano wa pili wa kilele kuhusu ushirikiano wa kimataifa wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” uliofanyika mwaka 2019, Wizara ya Fedha ya China ilitoa ripoti ya uchanganuzi kuhusu uendelevu wa madeni ya “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, hatua inayoonesha mtazamo wa wazi wa China kuhusu suala la uendelevu wa madeni. Kulingana na ripoti nyingine zilizotolewa na jumuiya za washauri bingwa, mpango wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” hausababishi kile kinachoitwa “mtego wa madeni”, na China siku zote imekuwa ikijitahidi kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na suala la madeni. Dkt. Ehizuelen amesema, ukweli unaonesha kuwa ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” unazisaidia nchi nyingi zinazoendelea kujitoa kwenye “mtego wa kutokuwa na maendeleo”.