Mawimbi ya joto yaikumba dunia kutoka Marekani hadi Ulaya na Asia
2023-07-17 21:53:39| cri

Makumi ya mamilioni ya watu wamekuwa wakipambana na joto kali duniani kote wakati utabiri wa hali ya hewa ukisema joto kali limetanda na kuweka rekodi katika maeneo ya Marekani, Ulaya na Asia, ukiwa ni mfano wa hivi karibuni wa tishio la ongezeko la joto duniani.

Mamlaka ya hali ya hewa ya Marekani imesema joto kali lililoanzia California hadi Texas lilitarajiwa kuongezeka, viwango vya joto wakati wa mchana vilitabiriwa kuwa kati ya nyuzi joto 10 na 20 sentigredi zaidi ya kawaida. Mjini Phoenix Arizona kulikuwa na nyuzi 43 mfululizo kwa siku 16, na kwenye eneo la Death Valley la California joto lilifikia nyuzi 54.

Barani Ulaya joto kali limeshuhudiwa katika miji mingi na nchini Italia katika visiwa vya Sicily na Sardinia joto limefikia nyuzi 48 sentigredi.

Nchini China mamlaka za hali ya hewa zimeendelea kutoa tahadhari kuhusu joto kali kwa baadhi ya maeneo kama ya mkoa wa Xinjiang joto kufikia nyuzi 40 hadi 45, na mkoa wa kusini wa Guangxi kufikia nyuzi 39 sentigredi.