Emir wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria tarehe 16 walifanya mazungumzo huko Doha, ambako walijadili namna ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya pande hizo mbili kwenye sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchumi, biashara, viwanda, nishati na teknolojia.
Kuhusu sekta ya gesi, nchi hizo mbili zikiwa ni nchi wanachama wa baraza la nchi zinazouza nje gesi asilia, zilijadili kuendelea kuimarisha mawasiliano na uratibu wa kisera kwenye masuala ya uzalishaji na uuzaji nje wa gesi asilia, na kubadilishana maoni juu ya masuala muhimu ya kikanda na kimataifa.
Rais Tebboune wa Algeria aliwasili Doha tarehe 15 kwa ziara ya siku mbili huko Qatar.