Mapato ya reli ya Ethiopia-Djibouti yaongezeka kwa asilimia 35
2023-07-17 08:41:30| CRI

Ofisa mkuu wa mkakati wa Kampuni ya Reli ya Ethiopia-Djibouti (EDR) Aminu Juhar amesema, reli hiyo iliyojengwa na China imesafirisha tani milioni 2.1 za mizigo katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 wa Ethiopia, huku mapato yakiongezeka kwa asilimia 35, na pia imesafirisha abiria 124,000 katika kipindi hicho.

Juhar amesema reli hiyo ina uwezo wa kupata dola za kimarekani milioni 60.1 katika kipindi hicho, ikiwa ni ongezeko la asilimia 35 kuliko mwaka wa fedha uliopita. Pia amehusisha ongezeko la mapato kutokana na bidhaa mpya kama vile magari.

Reli ya EDR ilianza safari kibiashara kwa kutoa huduma za usafiri wa abiria na mizigo tangu mwezi Januari mwaka 2018, ikiunganisha Ethiopia na bandari ya Djibouti.