Viongozi wa Afrika watoa wito wa mageuzi ya mfumo wa fedha wa kimataifa
2023-07-17 08:40:11| CRI

Viongozi wa Afrika wameanza mkutano wa katikati ya mwaka wa Umoja wa Afrika kwa washiriki kujadili maingiliano ya kiuchumi, na kutoa wito wa mageuzi ya mfumo wa fedha wa kimataifa.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Naibu Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi. Amina Mohamed amesema, wakati dunia ikiendelea kukabiliwa na migogoro isiyotarajiwa kutokana na athari za kiuchumi na kijamii za COVID-19, bara la Afrika ndilo limeathiriwa zaidi. Amesema ahadi zisizotimizwa zilizotolewa na jamii ya kimataifa za ufadhili wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na majimbo yasiyoridhisha ya masuala ya kibinadamu vimekuwa ni vikwazo kwa juhudi zinazofanywa na bara la Afrika na viongozi wake katika kutekeleza Ajenda ya Afrika ya mwaka 2063.

Amesema Umoja wa Mataifa unaungana na wito uliotolewa na viongozi wa Afrika wa kutengewa rasilimali zaidi kwa uchumi wan chi zao kupitia Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ambalo limekuwa likilaumiwa vikali na baadhi ya viongozi wa Afrika.