Rwanda yajenga vituo vya kuhifadhi gesi ya kupikia
2023-07-17 08:40:47| CRI

Rwanda imeanza ujenzi wa vituo vya kuhifadhi gesi ya kupikia (LPG) katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kigali, ili kuhakikisha upatikanaji tulivu wa gesi kwa watu wa mji huo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza matumizi ya kuni kwa kupikia.

Msimamizi wa mradi huo Jean Gashumba, amesema mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 32 utakaojengwa katika wilaya ya Gasabo, unatarajiwa kukamilika katikati ya mwaka 2025, huku kituo cha kwanza kikitarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja, ameongeza kuwa, mradi huo unafadhiliwa na serikali kwa kushirikiana na kampuni binafsi.

Waziri wa Miundombinu nchini Rwanda Ernest Nsabimana amesema, vituo hivyo vinatarajiwa kutuliza bei ya gesi ya kupikia nchini humo.