Mkutano wa tano wa uratibu wa katikati ya mwaka wa Umoja wa Afrika (MYCM) ulifanyika tarehe 16 mjini Nairobi, viongozi kutoka nchi kumi ikiwa ni pamoja na Misri, Gabon, Senegal, na mawaziri 51 wa mambo ya nje wameshiriki kwenye mkutano huo, wakijadili njia ya kuhimiza ujenzi wa eneo la biashara huria la Afrika na kuharakisha mchakato wa mafungamano ya kikanda barani humo.
Rais William Ruto wa Kenya alipohutubia ufunguzi wa mkutano huo, amesema, kwenye masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Umoja wa Afrika una uwezo wa kuchukua hatua muhimu za dharura barani Afrika kwa kutumia rasilimali zake.