Mwelekeo mzuri wa uchumi wa China hautabadilika
2023-07-18 08:36:36| cri


 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Mao Ning jana amesema, hali ya msingi wa uchumi wa China unaoelekea mwelekeo mzuri kwa muda mrefu haijabadilika, na kwamba Pato la Taifa la China (GDP) katika nusu ya kwanza ya mwaka huu iliongezeka kwa asilimia 5.5 kuliko mwaka jana wakati kama huu.

Akizungumzia athari ya uchumi wa China kwa sera ya diplomasia, Bi. Mao amesema siku zote China inafanya ushirikiano wa kirafiki pamoja na nchi mbalimbali juu ya msingi wa kuheshimiana, usawa na kunufaishana. Amesema China inaitaka Marekani ihimize uhusiano kati yake na China urudi kwenye njia ya maendeleo ya utulivu.