Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema, ukame wa muda mrefu katika Pembe ya Afrika umesababisha watu milioni 23.4 kutokuwa na usalama wa chakula, na watoto milioni 5.1 kupata utapiamlo mkali.
Shirika hilo limesema watu milioni 36.6 wameathiriwa na ukame katika eneo hilo, na kutoa wito wa kuchukuliwa kwa “hatua za haraka na za muda mrefu” ili kuzuia na kudhibiti athari mbaya zaidi na kupunguza matishio na hatari huku zikijenga na kuimarisha unyumbufu .
Pia limesema athari za ukame wa mwaka 2020-2023 zitaweza kuendelea kwa muda mrefu, na kwamba kutokana na hali ya ukame inayotokea kwa mara nyingi zaidi, itachukua muda mrefu kwa watu walioathirika kujijenga upya.