NMB, NBC kuunga mkono ajenda ya uchumi wa buluu.
2023-07-18 09:22:13| cri

Benki za NMB na NBC, zimejipanga kuendelea kuunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika utekelezaji wa ajenda ya Uchumi wa Buluu kupitia utoaji wa huduma bora za kibenki zinazokidhi matakwa ya wananchi.

Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti na viongozi wa taasisi hizo, baada ya kuandika historia mpya visiwani humo kwa kutoa mkopo wa pamoja wa Sh470 bilioni unalenga kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mwaka wa fedha wa 2023/2024.

Mkopo huo wa aina yake, Benki ya NBC ilichukua nafasi ya Mwekezaji Mkuu huku benki ya NMB ikiwa mfadhili mwenza wa mkopo huo ambao Serikali ya Zanzibar italazimika kurejesha ndani ya kipindi cha miaka nane.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Mwinyi amesema Serikali yake imepanga kutekeleza miradi ya maendeleo mara mbili mwaka huu ukilinganisha na miradi iliyotekelezwa mwaka uliopita kutokana na upatikanaji wa mkopo huo.

Amesema Serikali yake tayari imeweka mkakati kabambe wa kuhakikisha kuwa fedha za mkopo huo zinarejeshwa ndani ya kipindi cha miaka nane kama ilivyopangawa na kuwatoa hofu wote wenye wasiwasi juu ya Serikali yake katika la ulipaji.