Chama cha Mapinduzi (CCM) cha Tanzania kimeagiza korosho zinazozalishwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara, zisafirishwe kupitia bandari ya Mtwara ili kuzalisha ajira kwa wakazi wa eneo hilo, badala ya kutumia Bandari ya Dar es Salaam.
Kauli hiyo ya CCM inakuja ikiwa ni miaka kadhaa, tangu korosho zinazozalishwa katika Mikoa hiyo zisafirishwe kupitia bandari ya Dar es Salaam.
Mkwamo wa usafirishaji wa zao hilo kupitia bandari ya Mtwara, unatokana na kile kilichowahi kuelezwa na Kaimu Meneja wa Bandari ya Mtwara kuwa, yamekosekana makasha ya kusafirishia zao hilo, tangu ulipozuka ugonjwa wa Uviko-19.
Akizungumza katika mkutano wake na viongozi mbalimbali wa CCM Kanda ya Kusini, Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chongolo ameahidi katika msimu wa mwaka 2023/24 korosho zote zitakazozalishwa katika mikoa hiyo, kadhalika zitakazotoka Ruvuma.
Naye Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Atupele Mwakibete amesema katika bandari ya Mtwara yameletwa makontena mengi ambayo yatasaidia kutumika kusafirishia korosho kupitia bandari hiyo ambapo awali zilikuwa zikitumia barabara kwenda bandari ya Dar es salaam.