Biashara kati ya Kenya na nchi nyingine za Afrika yaongezeka huku wito ukitolewa wa maingiliano ya kikanda
2023-07-18 08:38:18| CRI

Biashara kati ya Kenya na nchi nyingine za Afrika imefikia rekodi ya juu ya dola za kimarekani bilioni 1.18 katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, ikilinganishwa na dola za kimarekani milioni 960 katika kipindi kama hicho mwaka 2022.

Takwimu mpya zilizotolewa na Benki Kuu ya Kenya jana jumatatu zimeonysha kuwa, ongezeko hilo limetokana na juhudi za serikali ya nchi hiyo katika kuboresha uhusiano wa pande nyingi na biashara kati ya nchi za bara la Afrika.

Benki hiyo imesema, mwaka 2022, mauzo ya bidhaa za Kenya kwa nchi nyingine za Afrika yalifikia dola za kimarekani bilioni 2.6, ikiwa imeongezeka kutoka dola bilioni 2.2 kwa mwaka 2021.